By Campos World
Poetry, sometimes ni private meeting ya just me and my paper,
Maneno za watu ni Kali kaa pepper,
Lawama nyingi zinaeza jaza pipa,
“Oyaa bro hauna talanta, unasound kaa stivo simpo boy”
Yea, nakujibu tu simpo, Freshi barida
Just maybe haujaniona Kwa hizo majarida
Siko Kwa interviews so unaniona Tu wa kawaida
Si hang na hao warembo, kina hamida na Frida
Yes, Hata Mimi nataka kufika
Hata Mimi nataka kusikika
Just maybe ni time haijafika
“Bro nasikia unajiita poet, aah bro wee si poet”
Yea mee ni poet, labda
Sipangilii maneno kaa hao wengine,
Sauti yangu inachokesha kuisikia pengine
Provided sijajipea crown ni mitaa Tu imenikubali
Lines nazo naungaunga, daily nikisali
Zinaeza zisikupee vibes kaa wengine
But atleast utapata originality na si copy kaa hao wengine
Maybe ni time Tu haijafika,
Sijui siku wala saa, sekunde wala dakika
But IPO tu itafika
Hata wewe utanisikia, la kufa dawa litasikia
Battle of words ita turn kua game of cards..
Ni true jina yangu hamjaiona Kwa awards
Sijui BET, AFRIMMA na GRAMMY
I Bet haijafika muda wanaendelea na prayers kina mom na granny
Just maybe ni time haijafika