Spoken Word

Haki Chaani

By Dee Olach

 

Kama kijana ntaishije maisha haya… maisha yenye hayanitambui maisha yenye kiongozi tulimchagua mwanaichi hata hamjui ..maisha ya lawama ya kijana anafaa kufanya na hata la kufanya hatulijui… Kazi kwa vijana pesa kwa wazee ati  nanii atanilee….

Kazi zenyewe haba hakuna vipi tutajaza hiki kibaba ,,,, nimengoja hizo kazi kwa vijana ulisema miaka imeenda ama ilikua propaganda tuu..

Swali ,,, vipi ntakidhi mahitaji??  juu life imenilemea natoa stress na mihadarati maisha magumu hata sijui nianzie wapi

Vijana tunataka kazi ata ka ujana ni moshi tumechoka na huu mwoshi wa sigara…

Na vipi kuhusu huduma za afya ,, jamii inacheleweshwa matibabu ama tuliwachagua ili mtupee adhabu.. Daktari anafokea mama wakati mtoto mahututi hajahudumiwa ..Na hizi bima za afya si mlisema matibabu ni bure.. Mbona wahudumu wanazembea anapita akiulizwa anasema “mwaache ule”

Watoto wanaranda mtaani vipi kuhusu ile elimu ya bure huku chaani

Kama kijana nina maswali mengi kichwani jibu langu ni kiongozi niliemchagua ata mtaani haonekani tutaishije

Tutaishije kama uhalifu umezidi tutaishije kama kazi na chakula akuna

Maofisini hatuezi pata haki bila hongo ati ,,, huduma hatupati mpaka mhudumu wa serikali umpe chai kinaya unatakaje chai na ata sisi wanaichi hatuezi pata hata mkate wetu wa kila siku huoni ata haya. ..

Mbona unibague na sisi ni wamoja ama unafurahikia hali hii ,, hali ya kubaguana ati wee ni nani huezi pata hii wee si Ali wee si wa hii jamii

I mean,,, sote ni wamoja tuungane tumalize hivi vihoja , mtoto aende shule, haki apate mama mboga, kijana apate kazi na kiongozi aletee maendeleo

Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu tushikane kuungane tumalize uhalifu, kukosa ajira, mihadarati na ubagi wa kikabila.

Related posts
Spoken Word

Nchi ya ahadi

Spoken Word

Swali

Spoken Word

THE MONSTER OF TODAY

Spoken Word

UNITE TO IGNITE

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *