NASKIA ANAITWA MOI
By Shesia the Poet
Haya Moi bila rungu hurumia walala hoi Maana wamechoka na wakiungana hutoboi Na hawatajali kama ni wa Bondo ama Sugoi Piga hatua za haraka wacha kuwa goigoi
Ni kubaya, sio mlima Kenya sio milimani Voi Sabina hajui acheke ama alie coz no more Joy Ju mali yake ilichomeka kwa lile soko la Toi Maskini anajaribu kujituma asife maskini
Na anapolalamika haskizwi kwa makini Wamekonda wengi they are getting more skinny Hivi mbona mnyonge hana haki!
Akiililia haki polisi wanamshika kwa hamaki!
Tena analimbikiziwa kesi za uongo baada ya kuwashtaki! Oyah skizeni kushikwa kiholela hatutaki!
Polisi tunawapenda ila vibaya mnatumiwa
Kuvuruga mikutano ndio mpate kusingizia watuhumiwa
D.O tumesubiri sana umalize mtu wa maziwa
Ama ilikuwa vice versa, kilio ni kwa watu wa miwa Tender ya kuimport sukari imepewa mhesh–miwa Vijana wamerudi kukaa maskani
Ni wasomi ila wanatafuta kazi na hazionekani
Wenyu mumewapeleka wakasomee marekani
Idle youths mnawatumia kupora kwa maandamano ili mlaumu wapinzani
Azimio walisema inawezekana mkasema haiwezekani Eti hakuna mkate nusu mara pap mkawaita mezani Oh kidogo kidogo bipartisan ikawashinda mizani
Sahii wapo kimya ni kilio tu mashinaniTunaumia sisi kwa sisi wakutusemea nani
Bunge la mwananchi nalo lina vita vya fulani na fulani
Oyah wazalendo hizo mlianza ni gani
Mlijichimbia kaburi wenyewe haya fukieni mpande maua
Si mlisema “my thief my choice” mbona mjute kuwachagua
Now hate yourself don‘t hate Ruto and gachagua
Tamu dole sambusa uamuzi wako usije kuua