Fumbo mfumbulie mjinga mwerevu alingamue
Ashakum si matusi so acha niwachanue,
Kuna wakulima wawili walikua na mbegu, dream zao zilikua ni wapate mazao sawa
Kampuni walikua nazo mbili na zote ziliahidi kuwapatia mbolea
Ili by the end of period X zile vitu walidream zingetimia
Mkulima akajiita mkutano, akapiga hesabu ni wapi angepanda mbegu
Na maybe angeongezea mbolea the seed ingenawiri na mazao angepata zaidi
Mashamba yakatayarishwa, mkulima akajituma, mbegu akaweka
Kampuni za mbolea zikajituma, maneno matamu pia wakatuma nayo watu waliotumwa kwa wakulima,
So mchanga ukachimbwa,mbegu ikatiwa kisha kufukiwa
Expectations zikiwa time ya kuvuna mkulima na familia ipate mazao ya kutosha leo kesho na hata milele. Na by the time wamwage mbolea, mbolea yenyewe ikue effective
Mvua ilipoanza kunyesha, ilikuja na fujo,
Kwanza kuosha mbolea
Pili kuchimbua mbegu, so ile ndoto ya kuchipuka na maybe mbegu kukua mti utakao faidi
Mkulima, watoto wa mkulima na watoto wa watoto wa mkulima iliishia
Time mvua ilinyesha.
Najua by 2027 tutakua na mashamba, lakini kurudia mbegu za 2022 itakua msiba wakujitakia
Nikweli tuliamini mbolea, but the truth is si mvua tu iliharibu mbegu but hadi mbolea ilichoma mbegu baada ya mvua kukatika,
Kampuni iliahidi chini ya siku kadhaa tungeona tofauti kwa mbegu zilizo wekwa mbolea
Miezi kadhaa imepita na hakuna dalili za mbegu kuchipuka
Ile mafuta ya sitini haijachipuka
Ilebima ya afya haija chipuka
Yule kijana kutoka slum atakaa kwa mlango juu ameshindwa na bei ya ufunguo wa maisha, education
Mwenye mbegu ni kila mkenya wa 18+, na mashamba ni zile sanduku hupangwa tukivote
Wenye mbolea forever itabaki kuwa chama na candidates wao
Its high time tukubali hakuna mtu atatulazimisha kupanda mbegu kwa shimo hatutaki
So in the meantime wacha tuzidi kuvuna mazao
Ule mti tulidhani ni mchenza, umegeuka kuwa m-ndimu