By Campos World
Nchi ya ahadi nchi Ilee..
Yenye wananchi hawapigi kelelee..
Eti gharama ya maisha imefika kilelee..
Ukiingia Kwa mall ukiona price tag mhhm ni masalalee..
Nchi ya ahadi, nchi Ile
Kama bustani ya eden ya adamu
Nchi yenye haina kumwaga damu
Amani inakuja na ncha ya kalamu
Wenye wako Kwa awamu
Wanatimiza malengo Kwa nidhamu
Tena Bila shutumu
Nchi ya ahadi
Nchi ya ahadi
Yenye nikisoma Kwa gazeti na kuona Kwa TV sikui sadi
Nchi yenye
Yenye wanasiasa hawatuchezi kama game na padi
Nchi yenye
Tuliowavotia hawatuonyeshi dasti
Nchi yenye
Nchi yenye youth Kwa uongozi anapewa chansi
Nchi ya ahadi Ile naionea mbali.