Spoken Word

ME NI LEADER

 

By  Alfred musinda –Campos world

(Naam, naam karibu bwana, nasikia aah unataka kua kiongozi na unataka kuongea na vijana wenzako je uko na kipi cha kuwaambia…ebu songea songea karibu uweze kushika kipaza sauti hiki uweze kuongea na vijana wenzako)

Voices

Atuambie nini, atuambie nini…uyo msee atuambie nini…

Bwana..Viongozi wako na suti na tai…wee umevaa nini??

“Buda uko mavitu

Unataka kua leader na hauna kakitu

Wee huoni hao wanatembea na ma body guard na ma pistu

Wana vitambi na wewe kamwili kako ka little…hahaha

buda Wee si leader”

Wee ni youth mwenzangu bro  already ushani downgrade…

Dreams umezirushia ma grenade..

Waliniambia ni dream big nishabuy kitanda ya 6 by 6..

Vitu nishajiingiza sijali kaa zitanipeleka kwa ground 6 feet..

Mee ni youth, healthy and soo fit, mbona nisikue leader..

Najua mna expect wale wenye mafedha..

But after 2 months mshaanza kulia na ma corrupt nation..

Najua tunaishi kwa corrupt nation na generation ya full of vision na ambition..

But si zote huishia tumboni mwa mwenye nchi..

Apo si ndio hujua difference ya mwenye nchi na mwananchi..

Wengine wakilala bungeni, kwengine wakikua impeached..

So adi niraise hii voice sijali ata kaa itakua na low pitch..

Youth sio leaders wa kesho..

Si tunarise leo..

Mee ni leader jooh..

Sisi ndio kioo ya jamii, tunafaa kuiokoa na sieti nini..

Nikitaka votes mtanipee..

Ama mtanidharau mee ni msee hivihivi..

Nadai kuwaongelesha si msongee..

Mkuje msikize izi mada heavy heavy..

Mee ni leader.

Voices

Aaah umesikia uyu jamaa…utu ako na point na sieti nini…mayouth tumelalisha mbaya…uyu jamaanitampa kura..

Enyewe, enyewe, enyewe, enyewe walai tena siuongo..walai walai…

Related posts
Spoken Word

PRA TREE

Spoken Word

Ngeli ya TU

Spoken Word

NA-JUA

Spoken Word

MGALA MUUE...

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *