Human Rights

Wape watoto haki zao kwa kesho bora

Watoto ni baraka kutoka kwa Maulana na ni wajibu wetu kama jamaa na jamii kuwalinda. Visa vya watoto kutelekezwa kila uchao vinahuzunisha na kukatisha roho. Watoto wengi wamenyimwa haki zao si Kkenya tu bali duniani kote. Katiba ya Kenya inamtambua mtoto kama yeyote aliye chini ya miaka kumi na minane ikiwemo ata yule aliye tumboni mwa mama yake. Kulingana na katiba, mtoto ana haki ya kutambuliwa kibinadamu na mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu na huduma za afya. Mtoto ana haki ya kidhirikiana na wazazi wote wawili na kutobaguliwa kwa minajili ya rangi, jinsia, uraia, dini au kabila. Watoto wanahitaji kulindwa dhidi ya madhara na uhalifu. Haki za watoto zinalenga kuwapa watoto uhuru wa kimwili na kiakili dhidi ya kunyanyaswa. Na ili astawi, mtoto ana uhuru wa kucheza na kuburudika.
Kila uchao tunashuhudia akina mama wakiavya mimba na kuwanyima wana wao haki ya uhai. Ingawa mama hawa wana sababu zao hawana uhuru wa kuyakatiza maisha ya watoto ambao hawajazaliwa. Mara kwa mara vijakazi huzozana na waajiri wao na kupelekea mtoto au watoto kulipia kwani fahari wawili wakipigana nyasi ndizo huumia. Yaya hawa huwatelekeza watoto au ata kukatisha uhai wao. Si haki mtoto kulipia madhila ya wazazi wake, vijakazi wanafaa kutafuta mbinu mbadala ya kupatana na kusuluhisha matatizo yao.
Wale wanaofaa kuwalinda watoto wamewageuza mawindo kwa kuwabaka na kuwalawiti. Baadhi ya waathirika ni wachanga mno kubaini kilichowatendekea hivyo kupelekea sheria kutofuata mkondo wake au kama mzazi au jamaa anahusika, mtoto ukanywa dhidi ya kumweleza yeyote au kunyamaza tu ili kulinda hadhi ya jamaa hao. Ni hatia na washukiwa wakipatwa na hatia wanafaa kuadhibiwa vikali.
Wazazi wanapoaga dunia jamaa na marafiki huachiwa jukumu la kuwalea watoto wa marehemu. Wengi utafuta njama za kujinufaisha kupitia mayatima. Badala ya kuwalea na kuwatimizia mahitaji yao wanawafanya vijakazi na kuwaadhibu vikali wanapokosea. Jamaa hawa wanasahau mayatima ni watoto kama wao na wana haki sawa na wana wao. Watoto wengi wameshindwa kustahimili madhila haya na kugeukia ndoa za mapema au kuingilia ukahaba ili wamudu maisha yao na labda wangepelekwa shuleni wangekua wahandisi, madaktari na viongozi wema. Wengi wanaweka tamaa kabla ya utuwema. Jamii nayo imelegeza kamba na badala ya kukemea tabia hii wanaipea kisogo kwa kuwa haijawafika.
Katika watoto wa mitaani baadhi yao waliacha shule kwa mapenzi yao. Wanapofika kiwango cha kujua baya na zuri wanajifananisha na wazazi na kutowatii. Wanakimbilia mitaani na kutumia dawa za kulevya. Maisha yanapowalemea wanageuka uhalifu wa kuwatishia wanajamii wapenda amani. Wanafaa watambue elimu ni haki yao na wazazi wamepewa jukumu la kuwaelekeza, elimu itawasaidia kesho na keshokutwa.
Nikihitimisha, wengi wetu tumekua watumwa wa mila na desturi, wafuasi wa kweli wa mwacha mila ni mtumwa. Baadhi ya mila zinakiuka sheria na zimepitwa na wakati. Ukeketaji wa watoto wa kike na baadaye kuwaoza zimepoteza ndoto nyingi na kusababisha maafa. Wadau mbalimbali wanakemea mila hii bali kunao watu kwenye jamii hawatilii maanani na kufanikisha mila hii kwa siri. Watoto wote wa kike na kiume wanastahili kutunzwa na kupelekwa shule. Ni wajibu wa kila mtoto kutambua haki zake na kuripoti panapostahili hakinyimwa haki zake. Kama vile mimea watoto wanahitaji kunyunyiziwa maji na kupaliliwa ili wakue. Kwa pamoja tudumishe na kulinda haki za watoto kwani wao ndio viongozi wa kesho.

About author

Caroline Boyani is a 20 year third year student in bachelor of Journalism and communication at The Technical University of Mombasa. She's passionate about telling human interest stories that cut across gender and democracy. She endeavours to be a multimedia investigative journalist with special interest in print media.
Profile
Related posts
Human Rights

Criminalization of civil society: A Slippery Slope for Kenya

Human Rights

Polls versus Human Rights

Human Rights

Bystander apathy and the rise of sexual violence in Kenya

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *