Articles

Changamoto zinazowakumba wamiliki wa biashara ndogo hususan wanawake

By Seliphar Machoni

Takriban watu milioni 62.1 wanamiliki biashara mbalimbali nchini. Milioni 7.4 ni wamiliki wa biashara ndogo na zinazokuwa kwa kiingereza, “small businesses and enterprises.” Idadi kubwa ya wamiliki wa biashara hizi wakiwa wanawake

Katika kaunti ya Kakamega, wamiliki wa biashara zinazokuwa ni zaidi ya asilimia 42. Licha ya kikundi hiki cha wamiliki wa biashara hizi zinazokuwa kujitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha kwamba wanaendeleza biashara zao ambazo zinawawezesha kupambana na gharama ya juu ya uchumi na maisha nchini, wanakumbwa na changamoto si haba hususan, wamiliki wa kike.

Wengi wa wamiliki hawa wanahofia kutoendelea na biashara zao wakilalamikia kutozwa ushuru wa juu zaidi ukilinganisha na hapo awali. Licha ya uchumi wa nchi kuzorota na kuchangia pia katika kufeli kwa biashara hizi, ushuru wanaotozwa wamiliki hawa ambao ni wakaazi wa kaunti ya Kakamega, wengi wao wanahofia kurejea nyumbani kwa kukosa pesa za kuendeleza biashara.

Zaidi ya kilomita hamsini kutoka mjini Kakamega, katika wadi ya Butsotso ya kati, soko la Eshisiru nakutana na Evelyne Lukongo ambaye ni mmiliki wa biashara ndogo na inayochipuka katika soko hilo. Evelyne alikuwa kwa shughuli zake za kawaida za kuuza mitumba na matunda ya kila aina katika kibanda chake kidogo cha mbao. Niliweza kuzungumza na Evelyne ambaye alikuwa tayari kunieleza changamoto wanazopitia kama wanawake wanaomiliki biashara zinazochipuka katika kaunti ya Kakamega.

Evelyne alinieleza kwamba anahofia kurudi nyumbani na kuharibika kwa bidhaa alizokuwa akiuza kama vile matunda na mboga kwa kukosa wateja, na faida anayopata kutoka kwa biashara yake ndogo- kulipia ushuru.

Kando na biashara zao kuathirika na mvua kubwa inayochesha eneo la magharibi, wamiliki hawa wanapaswa kulipa ushuru bila kuchelewa. Swala hili limeweka biashara zao katika hali ya  kuangamia. Kulingana na maelezo ya Evelyne, biashara yake imemsaidia sana katika kulipa karo ya wanawe, kukimu mahitaji yake ya kila siku na hata kulipia kodi. Kwa sasa anahofia huenda akafunga biashara yake kwa kukosa kupata faida na kukosa kulipa ushuru.

Evelyne anaeleza kwamba hapo awali walikuwa wakitozwa ushuru wa shilingi elfu mbili na mia tano. Tofauti na hapo awali walimiliki hawa wanatoswa ushuru wa zaidi ya shilingi elfu sita pasipo na kuzingatia aina ya biashara ambayo mtu anafanya- jambo ambalo wengi wa wamiliki wa biashara zinazokuwa wamelalamikia na kulikashifu. Kutokana na ushuru huu ambao unaendelea kuzorotesha biashara zinazokua, Evelyne, anasema kwamba hakuna faida wanayopata kutokana na biashara yao maana kidogo kile wanachopata wanalipa ushuru na kodi.

Evelyne anasema kwamba, kwa mara nyingi wamelazimika kufunga biashara zao siku ambayo wanapaswa kulipa ushuru kwa kukosa cha kuwapa wakusanyaji ushuru hao.

Anaeleza kwamba hapo awali walikuwa wanalipa ushuru kwa njia ya simu-“cashless revenue collection”; mfumo ambao uliletwa na gavana aliyeondoka mamlakani mwaka jana.

Evelyne alipongeza mfumo huo maana ulisaidia sana wamiliki wa biashara zinzochipuka kulipia ushuru kwa awamu pale wanapopata bila ya kuhangaishwa.

Analalamikia kuwepo kwa ufisadi katika shughuli nzima ya utozaji na ukusanyaji wa ushuru ambapo wamiliki wa biashara ndogo ndogo hususa wa kike wananyanyaswa sana na hata kutopewa muda wa kutosha wa kulipa ushuru huo.

Pia wamiliki hawa wanaomba kuwepo kwa uwazi na usawa katika utozaji wa ushuru maana kuna wale wanatozwa ushuru wa chini ukilinganisha na wengine. Kwa kusisitiza kauli yake Evelyne, Bi Mary, ambaye pia ni moja wa wamiliki wa biashara ndogo ndogo  katika soko hilo la Eshisiru, aliomba serikali ya kaunti ya Kakamega kuendeleza mfumo wa kulipa ushuru kupitia kwa simu-tamba  ili kuwawezesha kufuatilia kwa makini ushuru wao na kumuomba gavana wa kaunti hiyo kurudisha chini ushuru ili wamiliki wa biashara ndogo ndogo  waweze kuendeleza biashara zao na kujikimu kimaisha.

Waliomba serikali ya kaunti ya Kakmega kuweka mikakati ya kuwawezeshawa kuendelea na biashara zao hususa wamiliki wa kike pasipo na utozaji wa ushuru kupita kiasi ambao utapelekea kufungwa kwa biashara zao.

Wanabiashara hawa waliomba kuwepo kwa mikopo kwa wanabiashara wanaomiliki biashara ndogo ndogo ili waweza kuinua biashara zao na kujipatia kipato chao cha kila siku.

Related posts
Articles

Brian

Articles

Echoes of Midnight

Articles

Call for Action against Greedy Leadership: Gen Z Calls Them Out

Articles

Call for Peace in Kenya by President

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *