Articles

Nafasi ya mwanamke katika sekta ya teknologia na uvumbuzi

By Machoni Seliphar, Kakamega

Kwa miaka mingi sasa kote ulimwenguni wanawake wamekuwa wakipigania usawa wa kijinsia katika kila sekta ambayo wanakumbana nayo. Zimetokea kasumba kuwa yapo mambo ambayo mwanamke hawezi kuyatekeleza na zipo taaluma ambazo pindi tu mwanamke anaposimama na kusema kwamba yeye amebobea katika sekta hiyo kama vile uhandisi, ujuzi katika teknolojia na uvumbuzi wengi wanakuwa na mengi ya kuliza.

Kulingana na ripoti ya Pengo la Kijinsia ulimwenguni mwaka jana “Global Gender Gap Report 2022” kutoka katika World Economic Forum, ni dhahiri kwamba itakuchukua zaidi ya miaka 132 ili kupata usawa wa kijinsia ulimwenguni. Kando na hayo siku ya wanawake ulimwenguni imetangwa spesheli ili kuweza kutazana ni juhudi ganiu zimetekelezwa katika mchakato mzima wa kupigania usawa wa kijinsia wa wanawake.

Hapo awali wanawake wamekuwa wakijihusisha sana na tarakilishi kwa ajili ya ujuzi wao katika upigaji chapa ambapo kazi kama vile ukarani zilikuwa zimetengewa jinsia ya kike.  Maana zilisemekana kuhitaji ujuzi “mdogo” na hazikuwa na manufaa sana.

Kulingana na ripoti ya UN inayoonyesha dhahiri uwakilishi wa kijinsia katika uwanja wa teknolojia na mawasiliano ICT, uhusisho wa jinsia ya kike ni mdogo sana na asilimia 21 ukilinganisha na ule wa kiume. Hata hivyo zaidi ya wanawake asilimia 50 wanaojihusisha na maswala ya teknolojia wameripoti visa vya unyanyasaji. Ripoti hiyo pia inasema kwamba katika wale wanaomiliki simu za kisasa, jinsia ya kiume inaumiliki wa juu zaidi  kwa asilimia 18 ukilinganisha na jinsia ya kike.

Mwaka uliopita (2022), wanaume zaidi ya milioni 259 walitumia mtandao kikamilifu. Katika  taaluma ya teknolojia ni  asilimia 28 pekee ya jinsia ya kike waliohitimu katika kitengo hiki.

Machi nane kila mwaka ni siku ambayo imetengwa rasmi  kama siku ya kusherehekea juhudi za wanawake ulimwenguni. Mwaka huu (2023), kauli mbiu ya siku ilikuwa Uvumbuzi wa Teknolojia kwa Usawa Wa Kijinsia   “Innovation and technology for gender equality.” Dhana kuu ya kauli mbiu hii ikiwa ni kuchunguza  jinsi teknolojia imetumika katika mchakato mzima wa kuweka wazi changamoto zinazokumba wanawake kimataifa.  Wahusika kutoka katika mataifa mbalimbali walichunguza jinsi teknolojia imewasaidia wanawake katika mfumo huu wa kidigitali.

Nchini Kenya, elimu ya teknologia,uhandisi na uvumbuzi kwa wanawake na wasichana imepewa kipao mbele haswa kwa wale wanaotoka  sehemu  ambazo zimetengwa na ziko nyuma katika maendeleo. Maana wanawake na wasichana wakifunzwa njia mbali mbali za uvumbuzi  ni njia moja wapo ya kuwapa fursa ya kupambana na  hali ya maisha na kuweza kujikimu kimaisha. Pia elimu ya teknolojia kwa wanawake itawapa fursa ya  kupigania nafasi za kazi katika huu ulimwengu ambao umetawaliwa  na teknolojia na uvumbuzi .

Kutengwa , dhuluma na ubaguzi dhidi ya wanawake ni kilio ambacho kimekuwa   miaka 67 iliyopita siyo tu kisiasa, kijamii na kiuchumi,  teknolojia pia haijawachwa nje katika kuendeleza ubaguzi huu. Hili limechangia  sana kuwepo kwa siku ya ulimwenguni ili kuweza kuangazia athari  kubwa  ya  kutokuwa na usawa wakijinsia ambayo wanawake wamekuwa wakikumbana nayo katika jamii. Kando na hayo ni siku ya kuangazia mchango wa  wanawake katika jamii, uchumi na hata katika ulingo wa kisiasa  na kuangazia juhudi za usawa wa kijinsia.

Uwakilishi wa wanawake katika  vitengo mbalimbali vya ajira ni njia mojawapo ya  kuwapa wanawake fursa ya kudai haki zao katika kila kipengele cha maisha yao.

Ann Waiguru ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la magavana nchini akiwa katika mkutano wa IWD KICC “Kenyatta International Conference Center,”  alisema kwamba uwakilishi wa wanawake katika maswala ya  sayansi, teknolojia , uhandisi na hisabati  nimchache mno  na kutaka mikakati inayofaa kuwekwa ili kuzuia unyanyasaji wa mtandaoni kwa wanawake.

Katika kaunti ya Kakamega Prof. Janet Kasili ambaye ni mkewe gavana wa  kaunti Kakamega na mhadhiri katika chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro aliwahimiza wanawake kujiamini katika nyanja mbalimbali za kitaaluma, biashara na teknolojia huku akiwasihi kupigania haki na nafasi zao katika jamii.

Ingawa wanawake wakiafrika  wamepiga hatua katika maswala ya teknolojia na uvumbuzi bado kazi ipo, wanawake hawajapata uwakilishi wa kutosha katika tasnia hii. Bado kuna pengo kubwa katika teknolojia na uvumbuzi nchini Kenya na ulimwengu mzima, kuliziba pengo hili  ni wajibu wa kila mmoja kutafuta mbinu mwafaka ili kuliziba pengo hili.  Usawa wa kijinsia katika kila sekta nchini  ni haki ya kimsingi kwa kila mja duniani.

Kutambua vikwazo vinavyozuia wanawake kushiriki kikamilifu katika mfumo huu wa uchumi wa kidigitali itaisidia katika kutatua swala nzima ya uwakilishi wa wanawake katika sekta ya teknolojia na uvumbuzi na kuwapa wanawake  fursa ya kuwa mstari wa mbele katika mfumo mzima wakidigitali, teknolojia na uvumbuzi.

Related posts
Articles

Nairobi's Transformation: From Green City to Concrete Jungle

Articles

Kenya's Ongoing Battle with Malaria: Progress, Challenges, and Strategies

Articles

Mama Lucy Kibaki Eye Hospital Continues to Restore Vision

Articles

Empowering Obunga Fish Traders

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *