By Daniel the Poet
It’s so ironical maji ya kuosha mkono ni chafu kuliko maji ilimwagwa before tukule,
Tell me,sabuni ikichafuka utaioshaje,na daktari akiwa mgonjwa mbona asipelekwe
nyumbani?
Current state of the country ni blurry,kuna innocent blood humwagika everytime
tunademonstrate tuseme polisi wako na blurred-visson
Maybe dj should start from scratch, ndio tujue ni wapi tulikua na option ya kuruka mavi but
tukadecide turuke mkojo tukaland kwa shit
At some point naeza sema wale walifika chuo kikuu hesabu ya 1+1 iliwachenga 2022,so the whole thing ilianzia kwa ballot.
Tulidhani wanaelewa our pain juu tuliamini vitu walikua wakituambia siku za campaign , Festus wa mtaani hizo days alikua anaitwa festo,
Nakumbuka festo alipewa dooh agawie watu kumbe money festo alipewa ilikua icoverup uongo wangepublish kwa manifesto
Mara ngapi tumeambiwa heri shetani tunajua kuliko malaika hatujui…
Sai the whole country ni kilio,nothing is left on the right pia nothing right is left,so si
shakahola tu,but the whole country kinaturamba.
Mbona tulikataa elfu sita,ile pesa ya wajane na watoto mayatima ingekua imeingia,
Najua mtasema tulijipata kwa dilemma but ile bima ya afya kwa kila mkenya mmeipata?wapi
ile unga ya sabini na mafuta ya sitini?
Zile kazi za mavijana imegeuka kuwa stori ya evolution, from kazi mtaani to kupanda miti sai
tunaambiwa tungoje kuna plan ya kujenga manyumba…
A moment of silence for that nursing student mwenye atatumwa kwa site ya kujenga
Nabii atatuambia sheria zote za bibilia na kutuambia taifa la Kenya ni la wacha Mungu, but
kufanya kitu zakayo alifanya baada ya kushuka chini ya mti ndio haezi fanya,injili a anahubiri
ni ya ushuru.