Spoken Word

SAUTI YA MNYONGE

 

Naskia nduru na si kelele,

Kwa mbali naskia siren, then inafuatwa na maji but si rain….hizi ni lorry za polisi zinatumwagia maji

Naona vitoza machozi,polisi wametugeuka Niambie sabuni ikichafuka,utaioshaje?

Walivaa mask tusiwajue sura,
But because of the bullet na sare tunajua ni wao, Ni lini waandamanaji waligeuka kuwa magaidi? Naskia nduru za mama amepoteza kijana wake Kwa maandamano,
Naona comrades wa maseno kwa street,

Zile vitambaaza white sai ni red,

Ni mmoja wetu tumempoteza,but tukipaza sauti tunatawanyishwa na lorry za maji,

When did water become thicker than blood!

Ama all this is happening juu tuliambiwa amani haiji ila kwa ncha ya upanga?

Listen,all this is happening because so and so is pointing fingures juu ya figures tulisomewa sometime back in August,

Kama baada ya kura Kuna room for Dialogue,
Mbona watuforce kwa situation yenye our fellow die along before wakalie hizo viti,

Watatukumbusha vile uchumi ni mbaya na mafuta Iko juu but sisi tunaandamana kwa miguu wao wakikam na magari,

Ni mara ngapi watatukumbusha bei ya unga but wakiingia kwa mahoteli meal zao wanazidi kula kutumia uma na kisu!

Tumechoka kunywa vumbi mkiland na helicopter mkija tuwaambie vile tumesota, Tumechoka kukimbia kando ya convoy za magari zenu,

Tumechoka kuwaambia barabara zetu ni mbaya,ama juu mnaeza inua magari zenu ndio maana hamuezi tuelewa?

Kushoto ni wanafunzi wanaangushiwa bash but kulia Kuna wale wako njaa ju ya ukame,sijui mbona wanatuona washenzi,

Mhesh usidhani umekalia kiti Cha enzi,
Maskini ulisema utasaidia,mkono wa msaada fikisha Wenye njaa lisha,
Hii ni sauti ya mnyonge

DANIEL THE POET

Related posts
Spoken Word

Nchi ya ahadi

Spoken Word

Swali

Spoken Word

THE MONSTER OF TODAY

Spoken Word

UNITE TO IGNITE

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *