Spoken Word

Mate Chungu

By Dee Olach

Jua inawaka baridi pia, hello sijui ka bado mnaniskia, Okay ni Dee Olach atleast nimewaambia. Hii ni call away ya kule mbali nimetoka. Mi najiweza but road to success ni slippery so ni heri nirudi grao dry Ocha. Life ya kungangana kuomoka talanta imenikalia ka sofa. Hii life kweli si fair juu haijanipeleka mahali. Daily natry kuskuma atleast nieke chakula mezani. Life inaniadhibu kuniona mi mcanani still hopes ninayo ya kuvuka canan.Daily on my toes na bado life iko mbio kunikanyagia gizani. Deni ya rent nayo inaniandama ka yangu kivuli. Kelele ya token hainipi amani inaniambia tu nitoke niongeze juhudi.

Nasaka breakthrough day after day atleast niomoke ju mwili imekatalia kukubalia maisha ya toka nitoke. Life kunifather kwa uchungu hadi kunifanya mi niokoke  ju day after day natry kuovercome this life na damu ya yesukristo for this life ni uchungu nimeamua dilute na utamu wa yesu kristo. Daily msafiri tuu nikirudi road yangu ya success nikisaka funguo nilipoteza ya luck.Dooh chache nimeget inaisha bila plans najilaumu. Hii life kunikimbiza hainipi raha kunichokesha mwili na kazi ngumu. Daily akili kuchoka kuplan vitu haziwi thought yenye iko clear kwa kichwa pekee ni ile ya Kunywa sumu. Mi kusaka help but siezi pata ata ya jirani juu si deserve kwa wao kuniona mi kisirani. Kwani hii Baraka hupeanwa na nani?  Ni like life ya kusaka ladder niomoke imeniinvertia colours mi mwenyewe colourblind so ata sijui naonewa na nani. Hii life imenifunza nikuwe a lit generation ndo maana earlier nilikua nasaka niwashwe mshumaa. Life hard yenye siezi narrate ndani ya diary itafill up the pages. Kuskuma ivo ivo kumake sure life ninaifikisha to the edges. Sina backup plan yenye nikifail inibebe. Life ya kuzunguka na jua so kila jioni ni mimi na matembe za fever. Ama ni vile najifeel healthier kila time ndo maana life imekataa kunifever. Juu hii life ya pombe apana nimekataa kuchoma liver. Life ya shule kunifungulia jela ya maisha ingine as a form 4 leaver.

Jobless me but crime kwangu si option natry adopt my life sina furaha ka mtoi wa adoption okay, sina option ndo maana nimeamua talanta akue Bae.

Natry my best atleast hii position niondokee. Nimechoka kujifather atleast nipate mwenza anilee ndo maana niko up on my toes daily nimechoka onewa pia mimi nataka nijionee.

Related posts
Spoken Word

PRA TREE

Spoken Word

Ngeli ya TU

Spoken Word

NA-JUA

Spoken Word

MGALA MUUE...

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *