By Shesia The Poet
Tunacelebrate mashujaa wa zamani , wenye walipigania uhuru na amani
But walituacha kwa hands za thieves dressed in suits agenda yao ni
HI MONEY
Kuna brighter days kweli? Wacha tukeep Imani ,hakuna uhuru
So tunacelebrate our parents instead
The health workers wenye wamefight through thick and thin
Bila mshahara, wale wasanii wameshika upcoming artist mikono
Siasa place pia kwa kuonyesha youth kwa siasa your voice matters
Leo ndio tunacelebrate 60years of independence
But Kenyans hawachangamki, juu ya high pay tax
Wanaworry ni nini watakula adhuhuri
Waswahili husema not yet uhuru which is true
Kenyans wanalive in the past ,wanastruggle na neo-colonialism
NASKIA SAUTI, NASKIA SAUTI
Naskia kilio cha mababu zetu walio pigania uhuru wa taifa hii
Kinaya ni kuwa uhuru tunaye licha ya sisi wananchi
Kukatwa ushuru wa hali ya juu
Wimbo wa mzungu aende ulaya mwafrica apate uhuru
(maumau) upo wapi kwa sasa
Viongozi waliutwa ulafi na kuwa mabeberu Weusi
Ni mara ngapi tumeskia mali ya umma imeibiwa
Msemo uliopo ni pesa kwa wazee kazi kwa vijana
Miaka zaidi ya hamsini tangu nchi yetu kudaiwa k upata uhuru
Licha ya ufisadi kuwa hali ya juu
Ufisadi nchini imekua kama zao la fedha
Kila mwaka sisi husherekea siku kuu ya jamhuri na mashujaa
Ila ushawahi jiuliza pana shujaa yeyote katika enzi hii?
Wanasiasa ni wale wale ,miaka kumi uongozini
Hakuna maendeleo ,na ahadi waliyoahidi
Hakuna hata moja yaliyotimizwa na bado twasema tano tena
Ndugu zanguni wakenya ni lini tutakaa kufanywa vibonzo
Hebu tuamke na tukatae uongozi uliooza wakenya
Hebu tuamke na tukatae uongozi wa ukabila