
By Daniel the Poet
Walipigia affordable housing debe,
Kwa streets tulibaki tukipiga kelele
But interpretation ya leaders walituchukulia kama empty debes
Waliignore sauti zetu I guess tulikua tunawapigia kelele
Serikali imeamua kila mkenya apewe
Juu ni wao ndio wako na finance bill
Asubuhi ukiamka unashindwa kunywa hata chai
Unatamani enzi za serikali ya nusu mkate
Hadi wale wamekua wakipaza sauti
Skuizi hawana say, waliacha kuitisha nusu mkate sai wako na shares ndani ya bakery
Na huko bungeni pelekeni vitanda
Waheshimiwa wakichoka kukaa wapande walale
Sitting allowance ni ndefu kuliko mshahara mwananchi anaingiza yet haikui taxed
Bunge imegeuka kuwa base ya laundry na contract walipewa na kampuni ya aerial
Design civil servants wanaoshwa,
Wale wanaitwa special sitting wanatoka wakiwa wasafi na mwosho mmoja tu
Juzi nikipitia peoples Daily ati sources zinareveal kuna mita 5 waheshimiwa walifiniyiwa wamuokoe
Sijui kama wale walimwangia shamba mchanga in the name of mbolea maswali yao yamejibiwa
Or maybe wale walibuy waste in the name of fertiliser sijui ka compensation iliwafikia
Ni kweli kenya is a god fearing country na ndio maana tunaishi in the days zakayo alikua mtoza ushuru
Tunataka verse tumechoka kuimbiwa chorus ya kulipa ushuru ni kujitegemea
Kwani ni mara ngapi tumeona wakipanda ndege kuenda kuomba msaada
Somebody tell christ aconcider kurudi kama mwizi
Maanake our pockets are empty
Ile gospel zakayo alipelekewa maybe kama kuna mtu ako na the recording ineza saidia
Hii ushuru imeokotwa for long
Its time wakenya waanze kurudishiwa kilicho chao mara nne