Si wanasema maisha ni shule na kusaka kazi ishakua assignment lazima ukue na papers sijui ka unaniunderstand…
nimeshinda nikiinstall paypal but nothing is paying pal..
Wallae kukosa kazi imenikalia kazi life imestand still but mimi I cannot withstand..
Siezi judge nikiona prostitution imerise she wants to make that little one happy atleast supper akule rice.. Nina that Degree nina hopes but nalack that employment am lost
Ni papers ngapi nimeleft kwa desk zenu kwani what am I not doing right…
Unemployment imenigeuza begger juu day in day out naomba kazi but response ya “Hakuna” ni basic na je needs..?
Walicome na pregnant promises za job but hawajai deliver or maybe bado ziko maternity on labour pain…?
So stress ya kusaka job imenifanya daily ni go for Johywalker ndo daily nikeep walking nisichoke..
Nowonder crime rates imezidi juu it’s alarming vile youth unemployed anataka nipiga ngeta just because nimevaa tai from a jobinterview ata sijawai..
Yaani.. youth ako bar na ako njaa no job ya kueka food kwa table but anacheers ama hii pombe inaeza liquor…. ?
So ata nimetoa hopes zangu kwa bakeries juu bila kazi sioni nikipata my daily bread,,
So kila interview wanasema watanicall na offlate unemployment imenifanya depressed and lonely sioni nikipata izo company calls…
Nimebaki nimejiblame ,, niko na papers nilivote but at the end nothing sina job….
Poet Dee Olach