WritAfrica

Imeandikwa na Alex Maina

Katika mtaa wa Eastleigh ulioko Kuinet Kapsuswa Ward, Soy Sub-County, wakaazi wanakumbwa na tatizo kubwa la utupaji taka ovyo. Takataka zimejaa kila mahali kando ya barabara, karibu na nyumba, hata karibu na maeneo wanakocheza watoto. Hali hii imefanya maisha ya wakazi kuwa magumu na yenye hofu kwa afya zao.

Hakuna mfumo rasmi wa ukusanyaji taka. Wengi hulazimika kuweka taka zao kwenye mifuko na kuzitupa kwenye mitaro au kwenye sehemu za wazi. Maeneo mengine sasa yamegeuka kuwa kama dampo. Harufu kali hutanda hewani, na mbu, panya na nzi hujaa maeneo hayo, wakiweka wakazi katika hatari ya kupata magonjwa.

Mama Achieng’, mama wa watoto wanne, anasema, “Hii hali ni mbaya sana. Kila siku tunahofia watoto wetu kuugua. Hata kupumua ni shida kwa sababu ya harufu. Tumejaribu kutoa sauti zetu, lakini hakuna hatua.”

Wakati wa mvua, taka hizi huziba mitaro, maji yanajaa na kuingia ndani ya nyumba. Wakati wa jua, moshi na vumbi kutoka kwa taka hufanya mazingira yawe magumu kuishi. Watoto hupatwa na homa, kuhara, na matatizo ya kupumua mara kwa mara.

Bw. Kiprotich, mkazi mwingine, anasema, “Tunahitaji msaada. Hatuwezi kuendelea kuishi na takataka kila kona. Hatuwezi hata kupumzika vizuri. Ni aibu.”

Wakaazi wa Eastleigh sasa wanaomba serikali ya kaunti ya Uasin Gishu iingilie kati. Wanaomba kuwa miundo mbinu mzuri iweze kuwekwa kuhakikisha Wakaazi wanaweza kutupa taka mahali ifaayo na pia waweze kuhamasisha wananchi kwanini ni vema kutupa taka mahali ifaayo. Wanataka kuwe na madampo rasmi, magari ya kukusanya taka mara kwa mara, na pia kampeni za kuelimisha wakazi kuhusu jinsi ya kutupa taka kwa njia salama. Wanasema suluhisho linahitajika haraka, kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Usafi si zawadi ni haki. Kila mtu anastahili kuishi katika mazingira safi na salama. Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kuwa mitaa kama Eastleigh haiachwi nyuma. Ni wakati wa hatua, si maneno. Eastleigh inahitaji kuwa mahali pa heshima, afya na matumaini kwa wakazi wake wote.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Before he came,
Kibos River Pollution
Tongues of War
The Cry of Lake Victoria Fishermen  
False Accusers
Station Magistrates

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.