WritAfrica

Walibeba ngao na mlinzi wezi hao

‎Saa tuko kwa streets tunadai haki yetu

‎Juu ni hao walisema haki iwe ngao

‎Na mlinzi nikaamini but bado ni hao

‎Hawataki haki inilinde wananihunt

‎Na polisi wananishoot marisasi (ati za mguu)

‎Nikiuliza wapi haki

‎Juzi wamenishow amount ya hongo

‎Imepungua nikashangaa ni gani hizi

‎Juu hongo ni hongo tu

‎Iwe ndogo au biggie, (ni kama kula fare

‎Si fair) juu ni hongo Ilizuia juzi mi kupata haki 

so saa hii sina ngao juu ni thao, thao tu nilikosa

‎Nimebaki napiga story vile mnyonge hana haki 

Unfortunately, huyo mnyonge ni mimi, you see.

‎Nimerudi kwa streets na kalamu na imani

‎Kuamsha jamii tusinyamaze tudai haki

‎Haki kwa kila mtu haki kwa kila kitu

‎Haki za kikatiba iwe haki kila siku

‎haki bila ukabila

‎Juu amani bila haki ni uwongo

‎Kama kumix ghetto na ubabini

‎Haiwezekani hiyo ni falacy kama combi

‎Ya Siasa na maombi (Catastrophe)

‎Amka tudai haki iwe ngao na mlinzi

‎Ndio tukae na undugu, amani

‎Na uhuru, raha tupate na ustawi

‎Nimechoka na nduru gizani sasa

‎Mi nadai haki inilinde ndiposa

‎Mi nionekaniwe na nuru hapa gizani

‎Nikisign out, nataka haki wala si tafadhali

‎Do you hear me


Camistare 2025

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Before he came,
Kibos River Pollution
Tongues of War
The Cry of Lake Victoria Fishermen  
False Accusers
Station Magistrates

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.