By Daniel the Poet
Skiza skuizi kila mtu anajiuliza na jua itawaka lini
Najua watu wengi wanadai kuwe na national prayer day wakenya wasaidike juu ya mvua
Ati because jua ilipokua mingi kuna viongozi waliomba
Najua mungu anajibu maombi, najua
Lakini najua kuna kitu najua hamjui
Viongozi wenu wanawajali sana ndio maana watafuatilia stori Za floods kwa news
Najua kuna viongozi flani baridi imewalemea wanalala kazini
Somebody tell Sakaja of course inawork
Yes zile uongo walipublish kwa manifesto
Yes zinawork
Walisema vile wakikalia hizo viti watatujali
Thank God floods ziliturelocate and upto this point no leader has come to our rescue
Najua mnaeza taka kuenda ata kwa ofisi muombe msaada
But si mnajua barabara zilizibwa na maji kiongozi haezi report at work
Najua tulimchagua Erick omondi kama rais ndio maana after amelaunch bridge kisii sai ako nairobi anaokoa watu naboat
Najua maybe floods hukam na mosquito so malaria si ajabu ikienda juu
But najua hii thought viongozi hawana ndio maana upto now net hazija anza kuwa distributed
Najua kuna committee itakua formed kuchunguza mbona drainage system zimefail
Najua kuna milioni kadhaa kama si bilioni zishatengwa kulipa wale wote waliathirika na mafuriko
But najua hizo pesa hazitawafikia juu si viongozi walileta mvua
Najua baridi ni mingi so viongozi wakilala kwa vyeo najua tutawaelewa,
Najua viongozi wetu wanategemea mungu sana ndio maana hawana haraka na mafuriko
Najua wanajiambia mvua ni baraka
Najua kuna death toll inarise juu ya watu kufa maji
But najua hio haishtui viongozi
Wana act polepole juu wanajua Dubai ndio mbaya
So najua next time wanasimama kwa press najua watatukumbusha vile tuko blessed.
Najua
Najua
Yes najua