By Daniel The Poet
Ni juzi tu, na watoto waisraeli walikua misri
Ni juzi tu, kilio cha wana israeli kilifikia maskio ya Mungu
Ni juzi tu, wana israeli walipaka milango damu malaika wa kifo asiwaue
Ni juzi tu, bahari ya shamu iligawanywa ikawa njia
Na ni juzi tu wakiwa jangwani Mungu aliwapigania
Inauma kuona familia kupoteza wapendwa wao kwa vita
Tell me, ni vipi waisraeli watafaidika kwa kuua watoto
Itakuaje Musa alikua nabii na hangeweza tabiri yale tunaona leo
Iteni Musa hapa atueleze mbona hakuskia sauti za waisraeli walipo taka kurudishwa misri
Because innocent blood Imemwagwa na waisraeli ni mingi
Mbona vita na chuki kati ya wanadamu, na we all suffer under the same sun
Ni lini mwanadamu aliwacha kuomba kwa Mungu through the son
Scriptures zinasema vita zetu si za mwili na damu
Lakini mbona naona stream ya damu ikiflow Palestine
Nani mzuri na nani mbaya…hakuna binadamu wote wako sawa
Our father who at in heaven,ulisema ukiitwa utaitika
Kwa niaba ya wapalestine tunainua mikono tukikuita
Open the heavens gate to receive watoto wako
Th innocent souls Israel inatuma kwako,
im sure they are pointing down to earth
Its time pia Palestine waokolewe from their oppressors
Ni kweli we don’t know the story
For the last time God kwa niaba ya wapalestine we are sorry come down waokowe kwa ngori