WritAfrica

MAENDELEO BILA HATARI: USALAMA WA WATOTO KWANZA

Imeandikwa na Alex Maina

Watoto wa maeneo ya Kidiwa na Uhuru Estate sasa wanakumbwa na changamoto kubwa kufika shuleni. Hii ni baada ya uhamishaji wa watu kutoka eneo la Kilimani na kufungwa kwa eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa nyumba za bei nafuu wa Kidiwa Kapsuswa awamu ya pili.

Kufikia shule jirani kama Union Primary, St. Patricks, St. Marys, na Township kunakuwa vigumu kwa watoto kutokana na barabara kuu zilizojaa magari ya yanayoenda kwa kasi kama matatu za umma na magari yanayopakia na kupakua mizigo. Barabara hizi hazina njia za watembea kwa miguu, na watoto wanapaswa kutembea karibu na magari hayo hatari.

Njia nyingine ya kufika shule ni ya kupitia daraja dogo la mto ambalo pia ni tatizo hasa wakati wa mvua. Maji yanapozidi kiwango, daraja hilo hufunikwa na maji mingi na watoto wanakuwa na hatari kubwa ya kupita wakihatarisha maisha yao. Hali hii inaleta wasiwasi kwa wazazi na jamii kwa ujumla. Kabla ya kufungwa kwa eneo hili, kulikuwa na barabara ndogo ndogo na njia za vijijini zilizowezesha watoto kufika shuleni kwa usalama na haraka zaidi. Njia hizi ndogo ziliwasaidia kuepuka barabara kuu na kupunguza umbali wa kutembea. Sasa, kutokana na uzio uliowekwa na njia hizi kufungwa, Watoto wanasababika kutumia njia hizi hatari ili waweze kufika nyumbani.

Mvua kubwa inaponyesha imekuwa ni jambo la kawaida kusikia kuwa watu wamepoteza maisha katika daraja hilo dogo, ambapo watoto na watu wengine walibebwa na maji wakati wa mvua kubwa. Hali hii ni hatari sana na haiwezi kuchukuliwa kama jambo la kawaida.

Tunaitaka Wizara ya Ardhi, kazi ya Umma, Nyumba na maendeleo ya Miji Pamoja na mhandisi au mkandarasi wa mradi huu, Mbunge wa Turbo, Mwakilishi wadi wa Kiplombe na jamii wafanye kazi kwa karibu ili kuhakikisha njia salama za Watoto zinapatikana. Watu wote hawa wanapaswa kushirikiana vizuri ili kuleta suluhisho endelevu.

Suluhisho zinazopendekezwa:

  1. Kutengenezwa kwa Njia Salama ya Watembea kwa Miguu – Ili watoto waweze kutembea kwa usalama kando ya barabara.
  2. Kujengwa kwa Daraja Imara na Salama linaloweza kuvumilia mvua na mafuriko.
  3. Kufunguliwa kwa njia ya muda Ili watoto waweze kufika shuleni bila hatari wakati ujenzi unaendelea.

Tunasisitiza kuwa, tunapaswa kuepuka ajali au maafa yatokee kabla ya kuchukua hatua. Hatua za kinga zinaweza kuokoa maisha na kuhakikisha watoto wetu wanafika shuleni vyema na kupata elimu kwa usalama.

Tukiendelea kuendeleza maendeleo, usalama wa watoto unapaswa kuwa kipaumbele chetu cha kwanza. Kufikia elimu hakupaswi kuja kwa gharama ya Maisha ya Watoto wetu.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Justice Is Just It
M-HONGO Ka-RUSHWA
Mambo si Barabara
IDentity Yetu
I Have Been Dreaming
The Killer Whale

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.