Kuja, kuja ebu kuja
Kuja nikuambie
Vitu zingine utasoma Kwa mitandao si kweli
Kuja nikwambie,
Uongozi huanza Kwa moyo si utapeli
Kuja nikwambie
Vile unafaa kusikiza wananchi si kuwakejeli
Kuja nikwambie
Uongozi ni kama fumbo
Ila usilifumbie mjinga
Huyo atajaza Tu Tumbo
Hoja za wananchi atapinga
Kuja nikwambie
Nikwambie vile hata mwananchi ako na jukumu kwa uongozi
Kwa hizo public participation
Wakitoa changizo tuwasikie
Kuja nikwambie
Uongozi Bora ni ule wenye kuna mshikamano
Usikue ule wa mamba kenge pia wamo
Kuwajibika tuongeze kwenye mabano
Kuja nikwambie
Uongozi ni Mimi na wewe
Usiwe na kiwewe