Nimekua Kwa Vita ya body na soul..
Thou Kwa mwili wangu sina ata muscle..
Mee na mabros tumeamua sii kuhustle..
Si Nvirii so siezi kua story teller
Struggle zina sauti Kaa soul…
Every night, every day bang bang..
Kwa shimo ya poverty ndio sii tumetoka..
Kustruggle Kwa hii life daily tumechoka..
Kuishi na mama kambo, daily akifoka..
Zikakufa adi dreams za kucheza soccer..
Si ni Hustler nation..
Cries zimegeuka thunderstorms
Na machozi yamekua rain..
Kwa hii reign..
Cheki na fumble Kwa demonstration nikikwepa bullets nikitry ku collect pieces za peace..
Yenye imeturn to pieces..
Ni matear gas tu
Wenye pesa wanasema haina presha..
Wao ni ma mansion zao Wana treasure..
Wahubiri wanahubiri amani na wameficha mapanga
Walikakaa Kwa Giza na kupanga
Leaders wanatudrive crazy
Ingekua gari tungekua tushapata accident
Milio ya bullets all over, yea axe imetupata imetuacha na dent..
Country tumeidivide….Wa kabila ingine haiezi decide
Kwa utengano tuna sleep over….
Eti wa cross* rift valley haezi cross over..
Eti omari haezi ingia Duka ya wafula hii imekua catastrophe
Na akiingia utasikia akiambiwa Kata-straw-fee
Tunahitaji Ku embrace peace, unity na togetherness
Alfred musinda
Campos world