Articles

AHADI ZISIZOTIMIA

By Gideon Juma

Ahadi ni deni, lakini hatuwezi kustahili. Chenye tumebaki nacho ni matumaini ya kuwa yatatimizwa ila mawazo yetu yamesonga mbele tukitazamia hali zetu kwa kuwa aliyemchagua amesahau ahadi zile alizotoa kwetu. Tutamlaumu nani kwa kuwa huyo kiongozi yuko usukani tayari na anatimiza malengo yake binafsi huku tuliomchagua tukisaga meno. Tumbo lake linapojaa wananchi wanasukumwa makombo. Wananchi wanaishi kwa uchochole kwa kukosa rasilimali na maendeleo mitaani. Miaka inapita, hali bado ipo palepale ilipokuwa bila mabadiliko ilhali aliyewapea ahadi anajaza ghala lake. Wanaporusha malalamiko yanabaki kuwa dua la kuku.

Tunasema aliye juu mngoje chini lakini baada ya miaka mitano wanaporudi chini watu ndio wale tunaosahau tuliyopitia na tunawarejesha kule juu tusizidi kuwafikia. Vilio vyetu vinakuwa kelele kwenye masikio yao. Tunapoteza imani kwa uongozi tulio nao. Wamekwama kwenye viti vyao hawataki kubanduka, nia yao ni kukaa hapo wakizidi kupora mali. Wameshasahau malengo yao waliyotazamia wakati waliokuwa wakiomba kura na kwa sasa hawajali wale ambao waliwapatia uongozi. Wanatarajia mafanikio kwa jasho la wananchi. Wamekuwa wenye nchi hakuna anayepinga nao, wanatumia nguvu kuwatuliza wananchi. Aliyekuwa mtetezi amekuwa mamluki, wanaofaa wawe karibu naye wamejazwa na woga. Tutakimbilia wapi sisi, kwa sababu popote tuendeko kuna moto. Kinachowahusu ndicho chenye maana kwao, wanawahadaa watu kwa maneno matamu.

Wananchi tusimame imara tujiunge kwa pamoja maana umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Tusimame wima tukiwa na malengo ya kiongozi tutakayemchagua sio kwa maneno bali kwa matendo, macho tuangazie kazi zao na tuwe na ufahamu. Tufungue macho yetu tuwe na mitazamo ya kufaidi maeneo yetu tukipinga uongozi mbaya wa viongozi. Sisi ndio wenye usemi lakini tumejidunisha tuwewape mamlaka watutawale badala ya kutuhudumia. Bila sisi hawawezi kuwa mahali walipo. Tushirikiane kwa umoja tupinge uongozi mbaya.

Related posts
Articles

Hii Serikali

Articles

Hii ni ya mapoliticians

Articles

BEAUTIFUL LIE

Articles

PROMISES ZA HUSTLER

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *