by Clifford
Kenya iko crooked…
Crooked mpaka ukisimama straight,
unaonekana suspicious.
Unawapandisha pressure
Kenya iko crooked…
Crooked mpaka
pastor anashika Biblia,
lakini hawezi shika job.
Kenya iko crooked
Serikali iko na mkono mrefu
Lakini kwa economy inakua mkono birika
Ama niseme ni mkono fupi?
Economy imefinywa
Inafanya Madem desperate
Wako na saloon na hawasongi
Kenya iko crooked…
Kanisani Tunahubiriwa Zakayo alishuka…
lakini bado taxes
zinapanda.
Demokrasia ni sauti, walitufunda.
Mbona leo wanatutenda kama punda?
Mizigo yetu, faida yao wamefunga
Katiba ndiyo ngao,
Uongozi ni huduma
Haki ni haki
Mbona haki imekuwa mzigo wa punda?
elimu ni ngao
Lakini mbona milango imefungwa
Juu pesa wanagawa gawa
Ama ni mi napagawa
Kenya iko crooked…
Tunafunzwa honesty,
lakini ukisema ukweli,
wanauliza,
“Wewe uko side gani?”
Na sii tamu utaulizwa we ni watamu ngapi?
Kenya iko crooked…
Kila campaign ni concert.
Kila manifesto ni Ndoto
Na si ndoto tu
Ni ndoto kwa kiti moto
Lakini uchaguzi ukigonga
Ni vurugu….
tunapigwa rungu
Risasi ya guu
Tunasahau sisi ndugu
volume inaenda mute.
Ama ni vile tuko na brain minute
Kenya iko crooked…
Tunajenga dreams,
halafu reality
inatuwekea detour.
Ama tumeingizwa illuminati
Juu lately imekukua 666
Mara after 6 months in the next s months
Kenya iko crooked…
Lakini swali
Swali ni…
ni lini sisi
tutaanza kusimama straight?
