Spoken Word

60 YEARS OLD KID

By Daniel The Poet

Miaka imezidi songa, lakini mtoto wa miaka sitini bado anatambaa

Ugonjwa, ujinga, umaskini unazidi tu pokonya our country men

The other day ilikua ndani ya mau mau na tulikua tunafukuza mabeberu

Ironically many years down the line after the struggles and torture we still want them back

Maybe ile redcarpet ilitandikwa ilikua inasymbolise damu ilimwagika time ya ukoloni

Lakini sielewi mbona tuliwaacha wasmile wakiitembelea

Mwaka ni 1964, na the enemies mababu zetu walipigana nao are no longer three but four

Ujinga,ugonjwa,umaskini na ufisadi

Mbona babu yangu ile shamba mzungu aliwachia kenyatta haijatufikia

Tunataka kujivunia kenya kuwa republic but hatuwezi

Imegeuka stori ya umbwa kula mtoto wake

viongozi wanazidi tunyanyasa

Ni nini cha kujivunia kama your grandparent hakupigana ndio kenya ikue jamuhuri

Inauma kuona hata wale walipigania, many years down the line na bado wanalia

Juzi mliona field marshal alipokufa ndio serikali ilingangana kurenovate nyumba yake

Many years down the line but bado kuna masquota

Many years down the line na bado serikali inahangaisha watu wake

Ile freedom ya multipartty after sec 2A kuwa repealed ilibaki kuandikwa tu kwa katiba

Skuizi wale wako na say ni wale wako kwa serikali tu

Mara ngapi tumeona wakenya wakitawanywa na lorry za kenya police juu wanakumbusha gava tuko kwa ngori, mtoto wa miaka sitini

Itakuaje serikali ni ya kenya lakini influence inatoka nje,

Itakuaje kenya inasonga mbele na  kujitegemea inamaanisha viongozi kukopa madeni mtoto wa miaka sitini

Ni kweli mabeberu walienda, lakini tulifukuza mabeberu ndio tubaki na mafisi

Viongozi kuallocate pesa ya kununua magari na kurenocvate maofisi

Yet walipa ushuru ni sisi

Watakuwa wa kwanza kutuambia kulipa ushuru ni kujitegemea lakini watazidi kututegemea

Tumechoka kuskia same names of people in every national holiday

Serikali iko na record ya majina zetu, pesa wametenga kufanyia sherehe

Just to showcase their new suits and vehicles na kutoa speeches ndefu, this time watuwekee kwa mpesa, for long izi sherehe zimekuwa za viongozi but wananchi pia this time tuwekewee za kupiga sherehe

Related posts
Spoken Word

Nchi ya ahadi

Spoken Word

Swali

Spoken Word

THE MONSTER OF TODAY

Spoken Word

UNITE TO IGNITE

Sign up for our Newsletter and
stay informed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *