WritAfrica

Wakaazi Wadai Hatua Za Haraka

Imeandikwa na Alex Maina

Mradi wa Kuboresha Makazi yasiyo Rasmi nchini Kenya, KISIP, ni mpango wa serikali ulioanzishwa mwaka 2011 ili kuboresha hali ya maisha katika makazi duni kwenye miji kumi na tano nchini Kenya. Malengo yake makuu ni kuboresha miundombinu na kuwapatia wakazi umiliki halali wa ardhi. Mradi huu unasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Miji kupitia Idara ya Uboreshaji wa Makaazi duni.

Mnamo Agosti 2024, eneo la Mwanzo liliingizwa kwenye Awamu ya Pili ya mradi huu. Waakazi walifurahia ujio wa mitambo ya ujenzi kama mashine za kuchimba, buldoza, malori ya mchanga, na rollers. Kazi ilianza vizuri ardhi ilisafishwa, ikasawazishwa, na msingi wa mawe ukawekwa. Hali hiyo iliwapa wakazi matumaini makubwa ya kupata barabara bora.

Lakini Kufikia Machi mwaka huu wa 2025, ujenzi ulisimama ghafla. Tangu wakati huo, hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika. Barabara imebaki katikati ya ujenzi, na sasa imekuwa chanzo kikuu cha matatizo kwa wakaazi.

Wamiliki wa magari wanalalamika kuhusu mawe makali barabarani yanayokatakata matairi, kuvunja vioo, na hata kujeruhi watembea kwa miguu. Mawe haya huruka magari yanapopita, na huwajeruhi watu walioko kando ya barabara na pia kuvunja vioo vya nyumba zilizo karibu na barabara.

Katika mikutano ya ushirikishwaji wa umma ya KISIP, Wakaazi wengi walitoa malalamiko yao. Mzee mmoja kwa jina la Macharia, machozi yalikua yanamtiririka akieleza kwa uchungu jinsi mradi huo umemletea hasara badala ya msaada. “Afadhali wasingeianza kabisa barabara hii kuliko kuiacha nusu; sasa inatuletea maumivu zaidi,” alisema baada ya kulazimika kununua kioo kipya cha gari kilichovunjwa na jiwe. Pia alinunua tairi jipya baada ya lile la awali kukatwa vibaya na mawe. Mama mboga mmoja aitwaye Nyaboke alisema amepoteza wateja kwa sababu kibanda chake kiko karibu na barabara na watu wanaogopa kusmama kando ya hii barabara. Alilazimika kuhamisha biashara yake ili kuepuka kupoteza kipato. Wazazi pia wameonyesha hofu kubwa, wakisema watoto wao wakitoka shuleni au wakitumwa dukani ndio walio hatarini zaidi kwa majeraha yanayotokana na mawe haya.

Wakaazi sasa wanatoa wito kwa Serikali ya Kaunti kupitia MCA wa eneo hili, mkandarasi wa mradi huu, na maafisa wa KISIP kuchukua hatua za haraka. Wanataka kazi ya ujenzi irejelewe na kukamilishwa bila kuchelewa. Barabara iliyokuwa chanzo cha matumaini sasa imegeuka kuwa hatari kwa Maisha ya wakaazi.

Jamii ya Mwanzo haitaki zaidi ya kile ilichoanzishwa; barabara bora na mazingira salama ya kuendelea na Maisha yao ya kawaida.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Justice Is Just It
M-HONGO Ka-RUSHWA
Mambo si Barabara
IDentity Yetu
I Have Been Dreaming
The Killer Whale

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.