Walibeba ngao na mlinzi wezi hao
Saa tuko kwa streets tunadai haki yetu
Juu ni hao walisema haki iwe ngao
Na mlinzi nikaamini but bado ni hao
Hawataki haki inilinde wananihunt
Na polisi wananishoot marisasi (ati za mguu)
Nikiuliza wapi haki
Juzi wamenishow amount ya hongo
Imepungua nikashangaa ni gani hizi
Juu hongo ni hongo tu
Iwe ndogo au biggie, (ni kama kula fare
Si fair) juu ni hongo Ilizuia juzi mi kupata haki
so saa hii sina ngao juu ni thao, thao tu nilikosa
Nimebaki napiga story vile mnyonge hana haki
Unfortunately, huyo mnyonge ni mimi, you see.
Nimerudi kwa streets na kalamu na imani
Kuamsha jamii tusinyamaze tudai haki
Haki kwa kila mtu haki kwa kila kitu
Haki za kikatiba iwe haki kila siku
haki bila ukabila
Juu amani bila haki ni uwongo
Kama kumix ghetto na ubabini
Haiwezekani hiyo ni falacy kama combi
Ya Siasa na maombi (Catastrophe)
Amka tudai haki iwe ngao na mlinzi
Ndio tukae na undugu, amani
Na uhuru, raha tupate na ustawi
Nimechoka na nduru gizani sasa
Mi nadai haki inilinde ndiposa
Mi nionekaniwe na nuru hapa gizani
Nikisign out, nataka haki wala si tafadhali
Do you hear me
Camistare 2025