WritAfrica

Ndugu yangu Kaa chini nikuelezee story,

Huko nilipo TOKA yani hali Sio shwari,

Na SI unamkumbuka dadangu alie bakwa na yule mbakaji SI Alishikwa na maaskari,

Kifungo alicho fungwa ni zaidi ya miaka kumi,

ila amini usiamini nimemuona Leo saa kumi,

Akiwa anapita hii mitaa ya ndani ndani,

Na mkono wake wa kushoto akiwa ameshika sabuni,

Nilishangaa sana mpaka moyo ukashtuka, 

Juzi tu ndio alihukumiwa eti Leo kashatoka,

Katika akili yangu nikahisi katoroka,

Ikanibidi nirudi Tena polisi bila kuchoka

Nilipo fika nikasalimia maafande,

Nikataka kuelezea nikashambuliwa konde,

Mmoja akaniambia kijana hebu toa ujinga hapa kabla hatujaanza kukufungia rumande,

Nilihuzunika moyoni niliumia, 

nilirudi nyumbani njiani nikiwa nalia,

Dadangu amebakwa na mbakaji ametolewa,

Nikichunguza vzuri kumbe pesa ndio inaongea,

So Kwa mana hiyo SI maskini hatuna nguvu,

Tukidai haki yetu Wana tumia vibavu,

Wanatunyanyasa sisi wafurahishe matajiri, 

Hawafanyi kazi wanafurisha  vitumbo na vishavu

Polisi wazuri wapo Hilo sikatai,

ila wingi ni wabaya wanapenda kujidai,

Na hawakusaidii mpaka uwape zachai,

Tunaishi na corruption dhulma wallahi,

Ni wengi wamedhulumiwa ila haki hawapati,

Serika wako bzy kuskiza wenye manoti,

Sisi walala hoi kesi zetu zinatupwa Kwa sababu hatuna kitu twaonekana ka maiti,

Japo haki sijapata still bado Nina uchungu,

Me naona hii kesi heri nimuachie mungu,

Niliongea mwanzo wakanipiga makonde,

Wasije wakanifwata wakanivalisha pingu

Ewe mungu yote SI umeyaona,

Maskini hatuna haki Kila upande Kila Kona,.dhulma zimejaa njaa zimejaa alafu wako bzy wanasingizia eti corona

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

False Accusers
Station Magistrates
The Rogue Officers
The Untouchable Estate Don
Kibuye Market Saga
 System Down: Patient Dead

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.