By Imani Freystar
Mum aliniambiaaa;
mambo si barabara
Juu Kuna leader Fulani hajaunda barabara
Na hata hajui kama ni MCA au MP
Na hajui atawafikia vipi
Hii road ya Huruma ward Haina huruma
Karibu ipeleke last born wetu ward after kujikwaa
Bruised by the hard rocks,
Harder than even lives zetu.
Magari yanakwama pia
Mvua kidogo kunaflood
Hakupitiki!
If only hii road ingeundwa
Life zetu zingelindwa.
Both the road na lives zetu zingenyooka.
We’d not worry about bad weather
Wacee wa boda hawangeogopa kupitisha customer kwa hii road
Na hatungelipa 100 place tunaweza lipa 50 bob.
Labda hata mat zingefika,
Tulipe mbao, tufike tao.
But for now, mambo si barabara,
Juu sina hata usalama kwa hii barabara.
Imani Freystar
The Midnight Star