Kinaya ni sisi kuwaita viongozi na bado tunatazama walinzi wetu wakibadilika kuwa wauwaji.
Walivunja amri ya uaminifu, Ile ahadi ya msingi,
Wakaacha damu ya wananchi ikitiririka barabarani bila hofu.
Wakati sisi tulikuwa tunawalilia, hao walikuwa wamesimama.
Wamewezesha kifo kiwe ndiyo Sheria mpya ya nchi.
Kinaya ni sisi tunawaita viongozi wakati kila Jina tunalotaja linajibiwa na kiza na vumbi la risasi.
Wanaongea kuhusu Amani kutoka kwenye viti vyao vya enzi.
Huku chini kimya cha maiti ndiyo ishara pekee inayoeleweka,
Mwili wa raia ni daraja la kupanda madarakani.
Kinaya ni karibu Kenya, hakuna matata lakini kwa nyumba hakuna nafasi ya kupita.
Tofauti Yao na hao ni Wild Beast.
Hebu tuimbe wimbo wa hakuna matata wakati mkondo wa uzima umefungwa na jiwe.
Wageni wanakuja kununua jua na milioni ya nyumba, lakini mnyororo wa hoteli umegeuzwa njia ya Mungu kuwa ngome.
Wanasema,” Tunauza uzuri wa Mara” Huku Sauti za kwato zilizopotea zikiskika mbali.
Wamechora mstari wa faida ya haraka katikati ya safari,
Na Ile hoteli ya kifahari imekua Jina ya laana kwa asili.
Kinaya!
Tunalinda chapa ya matangazo ya runinga wakati ukuta wa simiti unavunja sawa ya asili ya nchi.
Ni kinaya, our health is assured by God, lakini Siri za miili yeti sasa zimekua rehani ya dola, zikilindwa na Sheria za nchi za mbali.
Ni kinaya tunalala tukiamini mkondo wake wa uponyaji haushindwi lakini wanasayansi wa kigeni wanafungua Milango ya mifumo yetu.
Imani inasema: Afya ni zawadi isiyohitaji malipo
Soko linasema: Afya ni biashara inayohitaji data ya bure.
Kesho asubuhi taifa litaamka tena, na kinaya kipya kitaanza kuandikwa tena, kwa maana tunaita kinaya Sanaa, wakati kwao ni ratiba everyday.
