WritAfrica

Bwana yulee amerejea

Mkatili, mwongo, mpenda anasa

Kwa kweli, ina mkono mrefu

Yule tuliyemtimua amerejea

Amerejea na ni wa kisasa

Amerejea ana mtindo wa kisiasa

Baba yule ana mkono mrefu

Miguu kuivuka mipaka

Tukadhani mwenyeji

Tukamwona mwenzetu

Kumbe mwewe wa kuwachukua vifaranga

Kila kunakokucha nakiona kivuli chake

Kwenye majumba, hospitali magari na hata barabara

Bwana yulee mwenye kiu na njaa

Kapiga miayo hadi mchana

Amefura mdomoni kuwaliko wanaochana

Kwani ywazipenda za jaba

Kuna waliotimuliwa kwenye viti

Viti vya hospitali

Viti vya raslimali

Kuna walionyakuliwa vyeti

Vyeti vya serikali

Kuna waliopewa simiti

Chuma, reli na hata vitongoji duni

Kuna walioekezewa fedha

Pesa za raslimali

Kuna waliopewa Viti

Viti pesa na mali

Majumba yaliojengwa

Kwa pesa zilizotengwa

Kwa watu waliolengwa

Kwa malengo yasiyo mema

Kujitajirisha

Kujitayarisha

Maisha

Afya ya uchumi

Kuihatarisha

Kuna waliohamishwa makwao

Wengi kukosa makao

Amerejea yulee

Bwana tuliyemtimua

Amerejea na ni wa 

Amerejea na mtindo wa kisiasa.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Where Are the Leaders? Youth Rise as Insecurity Bites Manyatta B
Threading Hope: Kisumu’s Sh1.2 Billion Textile Revival Nears Completion
Rising Waters, Rising Voices: Nairobi Battles the Floods
A New Chapter of Hope as Ogwedhi School Launches Special Needs Unit
Residents Criticize Manyatta B MCA's Absence from Ward Office
Leaders and Partners Unite to Tackle Flood Crisis in Kisumu

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.