By Amelia Collines.
Mi ni mpenzi
Mi ni mpenzi si wa hii serikali
Juu ina sirikali
Mi ni mpenzi mtazamaji
Na tizama maji
Katika jiji la nairobi
A place of cool waters
Sai ni a place of pool of waters
Siri yao kuu ni kutupeleka Singapore
Na sai watu wanasink hapo
Mimi ni mpenzi si wa hii serikali.
Cheki Njoro sai anago low
Aki saka jah ndio asilale njaa
Huku Sakaja akija ni empty
Promises imejaa
Warsha yake sai imejaa
Si na magari ila imejaa maji
Millions of shillings gone
Down the drains na hakuna anaye jali
Wanasema ni ajali na pesa
Ya disaster management
Walikula bila kujali
Mimi ni mpenzi si wa hii serikali
Mimi ni mpenzi mtazamaji.
Sai Nairobi life ngumu
Juu ndio udumu
Lazima uwe na skills kama za samaki
Ama utashindwa kumiliki
Mshikaki, keki, pikipiki
Utabaki ukiwa kwa dhiki
Huku serikali na siri zao kali
Wakitamaliki kila kona kama wakatoliki
Sai options ya kusafiri nairobi ni tatu
Matatu, pikipiki na hata meli
Tumelia juu ya mia wengi
Wamepoteza familia
Pesa za disaster management
Bado wamekwamilia
Mimi ni mpenzi si wa hii serikali
Mimi ni mpenzi mtazamaji.
Nina mengi ya kusema
Kuhusu haya maji
Ila sai kuu ni kuwa yamemwagika
Na hayawezi zoleka
Wengi tumeteseka
Na kupoteza maisha
Wengi biashara zimeharibika na kuisha
Hatuna maisha ni kuisha tumeisha
Walofaa kutusaidia wanatudhalilisha
Hii siri ni kali lazima nitawajulisha
Juu hii term yao ikokaribu kuisha
Na itakuwa one term ama tukose maisha
Mimi ni kipenzi si wa hii serikali
Mimi ni mpenzi mtazamaji.
