WritAfrica

BARABARA MBOVU PATE

IMEANDIKWA NA AHMED KARAMA 

Kisiwa cha Pate, kilichopo Lamu Mashariki, ni moja ya maeneo yenye historia ndefu ya ustaarabu wa Kiswahili na uhusiano wa kibiashara na mataifa ya Kiarabu na Asia. Licha ya umuhimu wake wa kihistoria na kitamaduni, wakazi wa Pate wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa ya miundombinu, hususan barabara. Ukosefu wa barabara za kisasa na zinazopitika kwa urahisi umekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya kisiwa hiki.

Maendeleo ya kisiwa hiki yamekuwa yakikwamishwa na changamoto kubwa ya miundombinu, hususan hali mbaya ya barabara. Wananchi wa Pate kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuhusu barabara kuu ya Mtangawanda–kizingitini, ambayo licha ya kuidhinishwa kwa matengenezo, bado haijawahi kuimarishwa ipasavyo.

Zaidi ya miaka sitini tangu Kenya kupata uhuru lakini wakaazi wa lamu mashariki wanatamani kuona barabara ya lami. Barabara inayotoka mtangawanda kuelekea kizingitini ni barabara ya changarawe ambayo ni  nyembamba sana, na wakati wa mvua huwa na matope, jambo linalosababisha pikipiki na magari kushindwa kupita.

Kutokana na ubovu wa barabara ajali  za boda boda zimekuwa zikitokea mara kwa mara. Wengi wao wakihitajika kuuguza majeraha mabaya ambayo yangeweza kuepukika barabara ingekuwa kwa muundo mzuri.

Wagonjwa na akina mama wajawazito ni miongoni mwa watu wanaoathirika pakubwa na ukosefu wa barabara nzuri ya kupitika kwa urahisi. Wengi wao hupata shida kubwa kusafirishwa hadi hospitali kubwa za Lamu. Wakaazi wa maeneo haya hukosa huduma za haraka wakati wa dharura.

Pate ni kisiwa ambacho kitegauchumi chake kikubwa ni shughuli za uvuvi. Wavuvi hukadiria hasara kubwa kwa kukosa kufikia masoko kwa muda muafaka jambo ambalo linawarudisha nyuma kiuchumi.

Utalii, ambao ungeweza kufufua uchumi wa eneo hili lililo na historia ya kale, umedorora kwa sababu watalii wanakwepa kutembelea eneo lenye miundombinu mibovu.

Shida ya barabara katika Kisiwa cha Pate siyo tatizo dogo bali ni kikwazo kikubwa kinachozuia ustawi wa wakazi wake. Kukarabati na kuimarisha barabara ya Mtangawanda–kizingitini kutafungua milango ya maendeleo kwa sekta ya afya, elimu, biashara na utalii. Ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa, historia na urithi mkubwa wa Pate utabaki kufunikwa na changamoto za miundombinu duni.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

COMMUNITY EFFORTS VS CRIME
WHERE WATER PASSES
COMMUNITY GROWTH THROUGH SOCIAL HALLS
PASSPORTS IN A FLASH
The Habit of our leaders
Stop GBV

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.