WritAfrica

POMBE HARAMU MITAANI

Imeandikwa na Alex Maina

Chang’aa na busaa, pombe haramu ambazo zamani zilionekana kama burudani ya watu wachache sasa zimegeuka kuwa sumu inayoua ndoto, kuharibu familia, na kuua kizazi kizima katika maeneo ya Kambi Thomas, Kapchumba na Kilimani. Kila kona ya mitaa hii kuna kijana aliyepotea kwa sababu ya pombe. Mama analia mwanawe hajarudi nyumbani, baba analewa mpaka familia haijui chakula kitapatikana vipi, dada ameachana na shule, ndoto zake zikimezwa na ulevi.

Maisha yamebadilika. Si tena ya matumaini. Ulevi huu umeteka vijana wale ambao taifa lingewategemea kuwa walimu, madaktari, mafundi, au viongozi wa kesho. Badala yake, wanakunywa asubuhi, mchana na jioni, wakiishi maisha ya giza na mateso. Pombe haramu imewageuza kuwa kivuli cha watu waliokuwa  na ndoto kubwa wakiwa wachanga.

Lakini sasa, jamii imesimama wima. Wakazi wa mitaa hii wamesema TOSHA! Wazazi, vijana waliotubu, na viongozi wa kijamii wanalilia msaada kutoka kwa serikali. Wanataka kuona mabadiliko sio tu kwa maneno, bali kwa vitendo maana ahadi zilikua zimekua mingi zaidi ya jinsi vita inavyoendelea. Hapo awali ungeona wanapolisi wakikula hongo kutoka kwa wauzaji hawa hawa ambao wanawapoteza vijana kwa pombe haramu au wangewatia mbaroni kisha baadae ukirejea mtaani unawapata wauzaji hawa wameachiliwa.

Hivi karibuni, Chief wa eneo hili, Bi. Gladys, aliongoza operesheni kali ya kushughulikia wauzaji wa pombe haramu na kuwatia mbaroni. Watu zaidi ya mia moja walikusanyika kushuhudia pombe ikimwagwa, wauzaji Zaidi ya kumi wakikamatwa, na matumaini mapya katika maeneo haya yakizaliwa. Bi. Gladys alisema kwa ujasiri:

 “Hatutaruhusu pombe ichukue maisha ya vijana wetu. Tutasimama kama jamii na kusema hapana kwa biashara hii haramu. Nitawaongoza polisi na wanakijiji katika kila operesheni na kuhakikisha pombe haramu katika maeneo hii inazikwa katika kaburi la sahau”

Jamii sasa inatoa wito kwa serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuongeza juhudi. Wafanye operesheni hizi kuwa za mara kwa mara, wafungue vituo vya msaada kwa waathiriwa wa pombe, na wawekeze kwenye elimu na ajira kwa vijana. Maisha hayawezi kubadilika kwa kupiga marufuku pekee vijana wanahitaji njia mbadala za kujijenga.

Pombe haramu si burudani ni sumu inayoua kwa mpango na jamii ya Kambi Thomas, Kapchumba na Kilimani sasa inasema kwa sauti moja IMETOSHA! Wakati wa kuchukua hatua ni sasa na mshirikiano wa Serikali na wananchi utachangia pakubwa kumaliza kwa pombe hii haramu hapa mtaani.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

COMMUNITY EFFORTS VS CRIME
WHERE WATER PASSES
COMMUNITY GROWTH THROUGH SOCIAL HALLS
PASSPORTS IN A FLASH
The Habit of our leaders
Stop GBV

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.