WritAfrica

MTIHANI WA UONGOZI

Imeandikwa na Alex Maina

Tarehe 12 Septemba 2024, wakaazi wa Kapchumba na Kiplombe kwa ujumla walikusanyika kwa mkutano mkubwa katika Ofisi ya Chifu wa Kilimani. Mkutano huo uliandaliwa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo mpya ya chifu, na ulihudhuriwa na viongozi, wazazi, walimu wakuu wa shule, na wakazi wa eneo hilo. Mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa eneo hilo, Bi. Janet Rotich.

Wakati wa mkutano, Walimu wa shule ya Msingi na vilevile Shule ya Upili walipewa nafasi ya kutumbuiza jamii na mgeni mheshimiwa. Baada ya apo walimu wa shule hizi walipata nafasi ya kuleta malilio yao kwa mwakilishi wao.Ilipowadia nafasi ya Naibu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kapchumba alisimama na kumshukuru sana Mwakilishi wa Eneo Bunge kwa miradi ambayo amefanya awali katika shule yao kwa kuwajengea darasa la kisasa. Baada ya Shukrani Naibu Mwalimu mkuu alikua na ombi mzito kwa Mbunge. Alisema kuwa choo cha shule yake kiko katika hali mbaya sana na kinahatarisha maisha ya wanafunzi.

“Tusisubiri janga litokee ndipo tuchukue hatua,” alisema kwa msisitizo.

Alikumbusha hadhira kuhusu tukio la kusikitisha lililotokea hivi karibuni katika Kaunti ya Uasin Gishu. Tarehe 10 Julai 2025, katika shule ya Queen of Angels Academy, choo cha shimo kiliporomoka na kuwaua wasichana watatu wadogo waliokuwa wakikitumia. Tukio hilo liliwahuzunisha Wakenya wengi.

Naibu huyo alitumia mfano huo kuonyesha kwa nini ni muhimu kuchukua hatua ya haraka katika Shule ya Kapchumba. Alisema kuwa choo cha shule yake ni dhaifu na kinaweza kusababisha maafa kama hatua hazitachukuliwa. Wazazi waliokuwepo walimuunga mkono na kusema kuwa usalama wa watoto wao ni jambo la kipaumbele. Alimwomba Mbunge Bi. Janet kutumia fedha za Hazina ya Maendeleo ya Eneo Bunge (CDF) ili kukarabati au kujenga upya choo hicho cha shule.

Katika majibu yake, Mbunge huyo Bi. Janet alikubali kuwa suala hilo ni la dharura. Aliahidi kulifanyia kazi mara moja na kuhakikisha linawekwa kama kipaumbele.

 “Kupoteza mtoto ni uchungu mkubwa kwa mzazi yeyote. Hatufai kusubiri janga, lazima tuchukue hatua sasa,” alisema.

Jamii na viongozi wanapaswa kushirikiana kwa ajili ya usalama wa watoto. Wanafaa kuweka kipaumbele maisha na usalama wa watoto kama jambo muhimu lisilo na mjadala. Lakini sasa, kinachosubiriwa ni kuona kama kweli ahadi hiyo itatimizwa au kama ni janga jingine litakalotukumbusha kuwa tuliambiwa.

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

You Know We are Kin, I and You
The People’s Peace
Siasa Ya ID
UFISADI TIA  ZII
HEALTH SERVICE CHRONICLES
Protest is Not A Crime - Article 37

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.