WritAfrica

Shesia the Poet

Mhesh,

Nilirauka alfajiri,

Nilirauka ili nikuajiri,

Hicho cheo kisifanye utengane na maskini,

Baada ya kuwa tajiri,

Kaa ukijua ni tick yangu imekupa kazi,

Najua sahizi unapiga mahesabu ya kutafuta kijakazi,

Juu utabadili mtindo wa maisha kuanzia Kwa makaazi ,

Na hata mavazi

Mhesh,

Nakudai,

Nakudai kuanzia Leo,

Nakudai maendeleo,

Nakudai, haikuwa rahisi kuenda kituoni kukita kambi,

Nakudai usiende Tu huko kuongeza kitambi,

Usiende huko kuongeza dhambi,

Usiende huko kuongeza scandal hazibambi,

Usiende huko kupora,

Usiende huko kujifunza ukora,

Nenda utie fora,

Nenda ufanye niishi maisha Bora,

Nahitaji uchumi Bora,

Nahitaji elimu Bora,

Nahitaji tiba Bora,

Nahitaji Barbara mzuri na mengine mengi,

Ni haki yangu Mimi kama mlipa ushuru na mwananchi mzalendo,

Nishakupa kazi ili unifanyie kazi,

Ukizembea nitakupiga kalamu,

Ukizembea nitakupiga kalamu na Ile pen nlitumia kukuwekea tick.

Shesia the Poet

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Justice Is Just It
M-HONGO Ka-RUSHWA
Mambo si Barabara
IDentity Yetu
I Have Been Dreaming
The Killer Whale

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.